Kituo cha Usimamizi wa Masuala ya Familia cha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro Kikishirikiana na taasisi ya An-Nahl Trust Kimeendesha Mafunzo ya Ndoa kwa siku mbili kwa Walioko na Wasioko kwenye Ndoa. Mafunzo hayo yalifanyika tarehe 1 hadi 2 Januari 2022. Mafunzo haya Yaliwashirikisha Washiriki Wapatao 25 Kutoka Maeneo Tofauti ya Dar es Salaam na Morogoro. Washiriki hawa Walijifunza Mambo Yafuatayo:
1-Misingi ya Ndoa katika Uislamu
2-Uchaguzi Sahihi wa Mwenza
3-Uchumi wa Familia na Athari zake katika Kuimarisha Ndoa
4-Mawasiliano kwa Wanandoa
5-Sababu za Migogoro na Utatuzi wake
6-Nyumba ya Muislamu
Mafunzo haya Yaliendeshwa na Wawezeshaji hawa Wafuatao:
Dkt. Bilal Juma
Iddi Jengo